Jumatatu , 15th Jun , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea mambo makubwa saba ambayo Tanzania imeyasimamia kwa kusaidiana na nchi nyingine ama kuyaongoza katika miaka 10 wakati yeye alipokuwa Rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea mambo makubwa saba ambayo Tanzania imeyasimamia kwa kusaidiana na nchi nyingine ama kuyaongoza katika miaka 10 wakati yeye alipokuwa Rais.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, Rais Kikwete amesisitiza kuwa mchango huo wa Tanzania kwa maendeleo ya Afrika umekuwa ni heshima kubwa kwa nchi yake.

Miongoni mwa shughuli hizo ni Tanzania, kama Mwenyekiti wa AU, kusimamia uanzishwaji wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Afrika na nchi za India, Uturuki na Umoja wa Ulaya

Jambo la pili, amesema Rais Kikwete ni kuongoza Operesheni ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika kilichomwondoa madarakani Muasi Kanali Mohamed Bakar katika Kisiwa cha Anjouan na hivyo kulinda uhuru na umoja wa Visiwa vya Comoro.

Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za AU kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (2012-2014), Tanzania iliwezesha kubuniwa na kuliwezesha Bara na msimamo kuhusu tabia nchi na mpango wa kuutekeleza – Climate Change Concept Paper and Climate Change Action Plan.

Tanzania pia ilipewa nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Watu na Haki za Binadamu ya AU na Bodi ya Ushauri dhidi ya Rushwa ya Umoja wa Afrika.

Rais Kikwete pia amesema kuwa pamoja na viongozi wengine wa Afrika, Tanzania ilifanikiwa kuanzisha Umoja wa Viongozi wa Afrika wa Kupambana na Malaria na Rais Kikwete mwenyewe kuwa Rais wake wa kwanza.
Imetolewa na;