Maandamano hayo yalipelekea vifo vya watu takribani 25 wakiwemo Askari Polisi 5
Raia wa nchi hiyo walikua wanaandamana wakipinga maisha kuwa magumu, rushwa na ukatili wa polisi wa nchi hiyo
Rais Julius Maada Bio amesema kuwa licha ya baadhi ya askari polisi kutokua na weledi lakini maandamano hayo yalikuja kwa kushtusha na kupeleka nguvu nyingi kutumika
Rais Bio ameulaumu upinzani wan chi hiyo kwa kujaribu kuitikisa serikali yake , madai ambayo yanapingwa na upinzani wa nchi hiyo
Ameongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua ukweli wa maandamano hayo
Amesema baadhi ya waandamanaji walikua wanawachochea watu kufanya mauaji na kuwashinikiza wanajeshi kuingia ikulu ya nchi hiyo
Rais huyo ametetea maamuzi yake ya kufanya mabadiliko kwenye jeshi la nchi hiyo baada ya maandamano hayo huku akikanusha tishio la kupinduliwa