Kipindupindu chabisha hodi

Monday , 17th Jul , 2017

Serikali ya Kaunti ya Nairobi nchini Kenya imeanza operesheni ya kufunga migahawa ya kuuza vyakula ambayo haina leseni hasa vibanda vinavyopatikana pembezoni mwa barabara.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya watu thelathini wakiwemo Mawaziri wawili kulazwa hospitalini baada ya kubainika kuwa na dalili za ugonjwa hatari wa kipindupindu.

Afisa wa Afya katika Kaunti hiyo Daktari Bernard Muia amesema vituo visivyokuwa na leseni vitafungwa katika jithada za kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Aidha, Daktari Muia amewataka wafanyibiashara katika jiji hilo kuwa waangalifu kuhusu vyakula wanavyowaandalia wateja wao na kudumisha usafi wa hali ya juu ili kuepusha maambukizi.

Watalaam wanasema kuwa, uhaba wa maji jijini Nairobi ni chanzo cha mlipuko wa Kipindupindu ambacho hata hivyo Wizara ya Afya nchini humo imedai kuudhibiti .

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi