Ijumaa , 30th Sep , 2022

Kesi iliyofunguliwa na Halima mdee na wenzake 18, ya kupinga kuvuliwa uanachama wao na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imeshindwa kuendelea leo kutokana na Mawakili wa washtakiwa namba mbili na namba 3 kutokifika mahakamani.

Wabunge waliovuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Hayo yameelezwa na Wakili wa upande wa waleta maombi Edson Kilatu, mara baada ya kiahirishwa kwa kesi hiyo, huku akibinisha kuwa mawakili hao wametoa taarifa kwa mahakama kuwa wameshindwa kufika mahakamani kutokana mkutano wa mawakili wa serikali walioufanya siku ya jana jijini Dodoma.

Kesi hiyo namba 36 ya mwaka 2022 inayosikilizwa mbele ya jaji Syprian Mheka imefunguliwa dhidi ya mshtakiwa namba moja ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, mshtakiwa wa pili ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mshtakiwa namba tatu ambaye ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 7, 2022 ambapo wabunge wawili Grace Victor Tendega na Hawa Mwaifunga wataanza kuhojiwa na jopo la mawakili wa CHADEMA wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala kuhusu mchakato wa wao kuwa wabunge wa viti maalum.