JPM aombwa kunusuru mamilioni ya CUF

Tuesday , 10th Jan , 2017

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama Cha wananchi CUF Julius Mtatiiro amemuomba  Rais Jonh Magufuli kuingilia kati utakatishaji na uhamishaji wa fedha kiasi cha sh. milioni 369 za chama hicho, kutoka hazina na kuhamishiwa kwenye akauti binafsi.

Julius Mtatiro - Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF

 

Akizungmza leo na wanahabari  jijini Dar es salaam  Mtatiro amesema kuwa fedha hizo ni za Ruzuku ya chama,  hivyo zimehamishwa Januari 5 mwaka huu,bila ya kuwepo kwa taarifa kwenye bodi ya udhamini wa chama hicho,nakuziomba  mamlaka husika ikiwemo taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kufanya uchunguzi dhidi ya uhamishaji huo.

Kufuatia hatua hiyo CUF imeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na viongozi wa juu wa chama hicho,kuanza kukutana ili  kujadili kile alichokiita kuwa ni shambulio ili  kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu waliyohusika na  utakatishaji na uhamishaji wa fedha hizo.