Jumatano , 18th Mei , 2022

uelekea siku ya zimamoto kitaifa Mei 19, 2022 Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa kuzima moto Temeke likiongozwa na Mrakibu msaidizi Michael Bachubira limefanya ukaguzi wa vifaa vya kuzimia moto katika kituo cha Mabasi yaendayo mikoa ya Kusini cha Mbagala rangi tatu

Zimamoto wamebaini baadhi ya mabasi hayana vifaa hivyo huku vingine vikiisha muda wake wa matumizi.

Ukaguzi huo umefanyika kwa lengo la kuhakikisha vyombo vya usafiri vinakuwa na vizimia moto huku zoezi hilo likienda sambamba na utolewaji wa Elimu ya matumizi ya vifaa hivyo.

"Tumeamua kufanya ukaguzi maalum kwenye kituo hiki cha mabasi kwa kuwa hapa kuna magari yanabeba watu wengi hivyo tujiridhishe usalama wa abiria na mali kwenye upande wa majanga ya moto endapo yatatokea na je wanaelimu ya kutumia vifaa walivyonavyo" Alisema ASF Michael Bachubira - Kamanda Mkoa wa zimamoto Temeke.

Mara baada kituo hicho Ukaguzi pia umeendelea katika soko la Temeke stereo kukagua mifumo ya moto soko ambalo limejaa wafanyabiashara wengi pamoja na kutembea katika maeneo ya mama lishe akitoa maelekezo ya kuacha njia kwenye Visima vya maji maarufu kama (FIRE HIDRANT)

"Hapa sokoni kuna mifumo ya maji na lengo la kufika hapa ni kujiridhisha na mifumo hii endapo inafanya kazi kwa usahihi kwa kuwa soko hili linakusanya watu wengi sana wafanyabiashara na wateja wanaofika sokoni hapa,hivyo niwaelekeze viongozi wa soko kuhakikisha njia za maji hazizibwi" alisema  ASF Michael Bachubira - Kamanda Mkoa wa zimamoto Temeke.

Kwa upande wa Uongozi wa soko la Temeke wamekiri uwepo wa changamoto sokoni hapo ikiwemo uwepo wa wafanyabiashara wengi wanaoziba njia wakiahidi kukomesha suala hilo

Siku ya kesho mei 19 wananchi wametakiwa kujitokeza Katika maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji viwanja vya Ilala Ili kupata elimu dhidi ya majanga ya moto na maokozi.