Hupati uwaziri kwa porojo - Katani

Friday , 19th May , 2017

Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmadi Katani amemponda Mbunge mwenzake kutoka Singida Magharibi Elibariki Kingu kwa kumwambia kuongea kwake maneno mengi ya kisiasa Bungeni siyo tiketi ya kupewa uwaziri na Rais Magufuli katika awamu hii ya tano

Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara, Katani Ahmadi Katani

Katani amesema hayo baada ya Mbunge huyo kudai kilichojaa kwenye hotuba ya kambi pinzani bungeni ni malalamiko tu hakuna 'altenative' ya nini kifanyike katika mustakabali wa nchi.

"Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. JPM siyo ukipiga maneno ndiyo anakupa uwaziri, hakupi uwaziri...Wote ukiwaangalia waliopewa uwaziri, unaibu waziri ni watu makini, wametulia siyo maneno maneno ya siasa. Sasa kama mnataka mnataka uwaziri kwa namna hiyo, uwaziri haupo na hakuna rishafo kwa bahati nzuri nimenusa...Kwa hiyo mnapokuja hapa muwe na hoja za msingi za kuishauri serikali". Alisema Katani

Pamoja na hayo Mhe. Katani amekili kuwa ni kweli kambi ya upinzani hawana mawazo mbadala katika kuishauri serikali juu ya kufanya ili iweze kuwa na maendeleo mazuri.

"Nikubaliane na wewe Kingu sisi wapinzani tutasema, serikali ndiyo inatekeleza  kwa hiyo unavyosema hatuna 'altenative' sisi hatupo kwenye mamlaka hayo kweli hatuna 'altenative' tutashauri tu... Nyie wenye mamlaka ndiyo mnawajibu sasa tunayoyashauri kuyafanya au kutoyafanya. Sitarajii tukija kwenye wizara nyingine mtapiga ngonyela hapa na kwaya zenu za vyama za siasa". Alisisitiza Katani