Jumanne , 29th Jan , 2019

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, ameitaja siku ya leo Januari 29, 2017 ni siku ya huzuni kwa demokrasia ya Taifa kutokana na kile alichokidai wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi kutumia wingi wao kwa hila kuamua kupitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Kushoto ni Mbunge Zitto Kabwe, Mbunge Upendo Peneza (Katikati) na Mbunge John Heche.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Heche amesema kwamba anapata hasira sana kwa CCM kutumia wingi wao kwa hila, kuamua kupitisha muswada ambao wao kwa kumtumia msajili wataamua nani awe mgombea urais wa chama fulani na nani awe Mwenyekiti na Katibu Mkuu.

Hata hivyo, Mbunge huyo amesema kwamba inasikitisha kwamba 'amendments' zote zilizokua zimepelekwa na wabunge wa upinzani kujaribu kurekebisha muswada wa sheria ya marekebisho ya vyama vya siasa zimekataliwa.

Amesema, "kuanzia saa 2:30  Katibu wa bunge hakupatikana kusaini 'amendments hizo ili zifanyiwe kazi".

Upande wa Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza amesisitiza kwamba "Schedule of amendments nyingi zimekataliwa. Tunasubiri kuona 'final schedule of amendment' ya serikali kama walau itakuwa imezingatia maoni na marekebisho yaliyofanywa na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge".

Kwa Upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe jana aliujulisha umma kwamba kuwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya sheria ya Vyama vya Siasa utaingizwa bungeni kesho na mjadala wa siku moja tu na kwamba jedwali la marekebisho la Serikali mpaka wakati huo (jana) walikuwa hawajauona.