Dhahabu yakamatwa ikisafirishwa kwenda Zanzibar

Thursday , 12th Oct , 2017

Mamlaka ya Bandari Tanzania, TPA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata madini ya dhahabu yenye uzito wa kilogramu 6.2 yenye thamani ya Shilingi milioni 500 katika bandari ya Dar es salaam ambayo yalikuwa yakisafirishwa kwenda Zanzibar.

Mkurugenzi mkuu wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Madini kutoka Wizara ya Madini, Bw. Tares Ngole, dhahabu hiyo ilikuwa ikisafirishwa na watuhumiwa wawili waliotambuliwa kwa majina ya Akifa Mohamed na Jafari Hussein

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amewaonya wale wote wenye nia ya kuitumia bandari ya Dar es salaam kupitisha bidhaa kwa magendo kwamba, mamlaka za ulinzi ziko imara katika bandari hiyo