Jumatano , 17th Aug , 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Maarifa Matala mwenye umri wa miaka 45, ambaye ni dereva wa daladala na mkazi wa Kimara kwa tuhuma za mauaji ya mtu aliyedaiwa kuwa mpenzi wake ambaye alikuwa ni kondakta.

Daladala

Akizungumza hii leo Agosti 17, 2022, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kutoroka na kukimbilia mkoani Lindi akidaiwa kumuua mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Sharifa ambaye alikuwa ni kondakta.

Aidha Muliro ameeleza kuwa katika hatua nyingine wamemkamata Gama Swai, anayetuhumiwa kwa kuuza spea za magari zinazodhaniwa kuwa vifaa vilivyoibwa kwenye magari ya wananchi.