
Mkuu wa wilaya Njombe Ruth Msafiri.
Mkuu huyo wa wilaya amesema hayo wakati akiwa katika ziara kwa shule za msingi za halmashauri zake tatu ili kuangalia maendeleo ya wanafunzi wanaofanya mitihani yao ya darasa la saba.
Bi. Msafiri amesema kuwa wazazi wengi wa mikoani hasa vijijini huwa wanawachukulia watoto wa kike kama vitega uchumi pindi wanapomaliza masomo yao ya msingi huku wakitoa visingizio.
Kwa upande wake wanafunzi wanaohitimu darasa la saba wamewaomba wazazi wao kuwaendeleza kimasomo baada ya kumaliza masomo yao ya elimu ya msingi na kutowatumia kama vitega uchumi na kuwaoza.
Nao baadhi ya waalimu wakuu wamesema kuwa wana uhakika wa wanafunzi wao kufanya vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari huku wakisema kuwa wamekutana na wazazi kuwasihi kuwaendeleza watoto wao.