Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mosses Machali amemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba na wataalamu wake kuendelea kufanya ukaguzi kwa wafanyabiashara ambao hawana leseni, ili ambao hawana wafuate taratibu na kupata leseni kwa mujibu wa sheria, na kuiwezesha serikali kupata mapato

Agizo hilo la mkuu wa wilaya amelitoa katika kikao cha siku ya pili cha baraza la madiwani, baada ya kutokea mvutano baina yake na baadhi ya madiwani, waliotaka zoezi la kukagua maeneo ya biashara na kuwafungia wasio na leseni lisitishwe, na wafanyabiashara waongezewe muda wa kulipia leseni zao.

"Nimewambia hapa kwa robo ya kwanza tumeshindwa kukusanya 30% ambayo ilikuwa lengo, tulikusanya 23%, hamna uchungu mnataka kuzuia maafisa wasiendelee kukagua wakati hizo haki zinatolewa kwenye kifungu cha 17 cha sheria ya leseni za biashara, mkuu wa wilaya au mamlaka nyingine inawajibika kuheshimu uamuzi wenu ambao unakidhi matakwa ya sheria" amesema Machali.