Jumatatu , 15th Aug , 2022

Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikianana wadau , taasisi na sekta binafsi katika kutafuta suluhisho la matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii haswa katika maeneo ya afya, elimu na huduma za jamii.

Mkurugenzi wa benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ameyasema hayo hivi karibuni mkoani Dar es Salaam kwenye mbio za marathon zilizoandaliwa na benki ya CRDB, mbio  zilizolenga kufadhili matibabu ya akinamama wenye ujauzito hatarishi, ikiwemo pia watoto wenye matatizo ya moyo, mbio zilizofanyika Oysterbay Masaki, ambapo zaidi ya wakimbiaji 6000 kutoka ndani na nje ya nchi walishiriki

"Ijapokua kwa sasa hatuna takwimu maalum kuonyesha idadi ya wanawake wenye ujauzito hatarishi, ila sote ni mashahidi kuwa hivi akribuni tumeshuhudia wakinamama wengi wakipoteza maisha kutoana na mimba hatarishi," amesema Dkt. Mpango

Aidha Dkt Mpango amezitaka taasisi na sekta binafsi kuendelea kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, akitolea mfano benki ya CRDB ambayo kupitia mbio hizo imeweza kutoa shiligi bilioni 1.

"Benki ya CRDB imekua msitari wa mbele kutatua changamoto za jamii, hiyo ni mbali na kutoa ajira na fursa mbalimbali, mpaka sasa CRDB imesaidia kutoa bilioni 1 kusaidia watoto wauaoumwa moyo katika kituo cha JKCI" ameongeza Dkt Mpango.

Mkurugenzi wa benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela, amesema kuwa benki hiyo inajivunia ushiriki wa wadau mbalimbali katika kusaidia jamii, ambapo mbio hizo zinazofanyika kwa mwaka wa tatu sasa zimekua zikiongeza idadi ya washiriki, ambapo mwaka huu zaidi ya washiriki 6,000 walipata wasaawa kushiriki na kufanilisha malengo ya kukusanya fedha.