Jumatatu , 24th Jan , 2022

Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe, amesema kuwa kundi kubwa linaloathirika zaidi na rushwa ya ngono na ukatili wa kinjinsia ni la wasichana wa vyuo vikuu sababu walimu wao ndiyo wanaoamua hatima za elimu zao.

Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 24, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kusema kwamba walimu wa vyuo vikuu ndiyo wanaoamua msichana afaulu ama afeli, tofauti na walimu wa elimu za chini ya hapo.

"Mwili wako ndiyo unaamua utoe rushwa, usipotoa rushwa utafeli ni mazingira ambayo magumu, tofauti na huku chini, huku utanifelisha 'coursework' lakini NECTA huendi kusahihisha wewe, lakini kwenye vyuo vikuu mwalimu anayekufundisha anaweza kuamua hatima ya elimu yako ni sehemu ambako mwalimu ana mamlaka mengi lakini anaweza kuyatumia vibaya yakamuathiri mtoto," amesema Massawe