Jumanne , 16th Aug , 2022

Makamishna wanne wa Tume ya Uchaguzi Kenya IEBC wakiongozwa na Naibu mwenyekiti Juliana Cherera, wameeleza sababu zilizowafanya kujitoa katika mchakato wa kutangaza matokeo ya uchaguzi nchini humo

Makamishna  hao wanadai  Mwenyekiti, Wafula Chebukati, aliwapindua na kusisitiza kutangaza matokeo licha ya wao kuwa na wasiwasi juu ya matokeo hayo

Aidha  wanadai kuwa kuwa hesabu ya mwisho ya matokeo ya uchaguzi wa urais haikuletwa mbele ya tume ili kushughulikiwa.

Sababu nyingine walizoeleza wamesema kuwa kuwa ujumlishaji wa matokeo haukuwa sahihi kimahesabu na kwamba matokeo hayo hayajumuishi jumla ya waliojiandikisha kupiga kura na kura zilizopigwa au zilizokataliwa

Tayari Raila Odinga ametangaza kuyakataa matokeo hayo leo