Changamoto ya makazi holela
Hata hivyo mtaalam wa mipango miji ambaye pia amehudumu kama Mkurugenzi wa Nyumba Wizara ya nyumba na makazi Kwa kipindi kirefu Prof Tumsifu Nkya ameeleza kuwa jambo muhimu kwenye upangaji wa miji ni takwimu sahihi za idadi ya watu kwenye Mji husika Ili kuepuka uholela unaojitokeza Kwa sasa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji na mtafiti nguli kutoka taasisi ya utafiti ya Repoa dkt Donald Mmari amesema kufikia mwaka 2030 Jiji la Dar es Salaam litakuwa ni miongoni mwa majiji makubwa Africa hivyo ni lazima sasa kulipanga upya Kwa mliangano sawa wa watu na mifumo ya huduma za jamii zitakazolinda utunzaji wa mazingira.
"Kwa sasa kasi ya ukuaji na upangaji wa miji ni ndogo kuliko kasi ya watu kuingia mijini hivyo ni wajibu wa taasisi za serikali wadau kuja na mpango kazi maalum na ndo maana tunafanya tafiti ili kuja saidia sera"alisema dkt Donald Mmari
Matarajio ya Watanzania wengi yameonesha Imani na unafuu mkubwa kiuchumi mijini tofauti na ilivyo vijijini Hali inayopelekea eneo Moja watu kuhamia Kwa wingi hivyo kusisitizwa uwekezaji wa kasi kwenye mipango miji hapa Tanzania.