Jumapili , 10th Oct , 2021

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ushetu Mkoa wa Shinyanga Bw. Linno Mwageni amemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Bw. Emmanuel Peter Cherehani kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Oktoba 9, 2021 Cherehani alipata kura 103,357 dhidi ya mshindani wake Bw. Mabula Nkwabi Julius wa ACT Wazalendo aliyepata kura 3,588 kati ya kura 106,945 zilizopigwa.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Elias John Kwandikwa ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi kufariki Agosti 2, 2021.