Jumapili , 9th Mei , 2021

Ngumi kali ya kati kwenda juu ya Saul 'Canelo' Alvarez ilitosha kumchakaza Billy Joe Saunders aliyefadhaika akishindwa kuinuka kutoka kwenye kiti chake baada ya raundi nane za pambano lao la kuwania taji la ubingwa wa duania la umoja ‘Unification bout’.

Pambano wakati likiendelea.

Baada ya Saunders kuachia mwanya, Canelo raia wa Mexico alirusha ngumi mithili ya risasi ambayo ilisababisha uvimbe wa haraka juu ya jicho la kulia la Bondia huyo wa Uingereza.

Mkufunzi wa Saunders aliamua kusimamisha pambano hilo, kwani bondia wake hakuweza kuona tena kwa wakati huo. Huku akishuhudiwa na watu takriban elfu 73,126 waliohudhuria pambano hilo Saunders alishindwa kabisa kunyanyuka kwenye kiti kuendelea na pambano hilo.

Saul 'Canelo' Alvarez akiwa na mikanda yake

Alvarez mwenye umri wa miaka 30 alisema, alipoenda kwenye kona yake ya kupumzikia alimwambia mkufunzi wake Eddie Reynoso kwamba anahisi amevunjika shavu kutokana na hali aliyokua akiihisi kwenye kimywa chake.