Ijumaa , 25th Mei , 2018

Kijana mmoja nchini Uganda ameshitaki kanisa moja nchini humo akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

Kijana Michael Aboneka amepeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church kwa madai kuwa linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda inavyosema.

"Kwanza wanasema nilazima upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu inakwenda na kinyume cha katiba kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua ya Daktari ya majibu ya kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa" Aboneka.

Ameongeza kuwa "Nimekwenda hospitalini kupimwa na mchumba wangu tumepata majibu tunafahamu majibu ya kila mmoja wetu. Kwa hiyo mimi na mchumba wangu kukabidhi vipimo vya ukimwi kwa kanisa inavunja haki ya uhuru wa siri zetu, nimekuta ni kinyume na katiba'. amesema Aboneka.

Aboneka ameongeza kusema kuwa siyo kanisa la Watoto pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini yanafanya hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja kusimamisha kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutoa jibu.

Aboneka amesema kuwa siyo kwamba ana chuki na kanisa la watoto, ila ni kusaidia vijana wengi ambao wameshindwa kufunga ndoa zao ili mahakama ya katibu itowe ufumbuzi wa swala hilo.