Jumanne , 29th Nov , 2022

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kupata ajali katika Kijiji cha Kitopeni Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida, huku mmoja akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Gaspar Itigi.

Moja ya gari lililopata ajali

RPC Singida Stella Mutabihirwa, amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Novemba 27, 2022 na ilihusisha lori na gari ndogo aina ya Mazda.

"Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu wawili papo hapo, na mmoja alifariki wakati anapatiwa matibabu, chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alihama kabisa upande wak na kulifuata gari dogo na kusababisha ajali hiyo," amesema ACP Mutabihirwa