Jumatano , 20th Jul , 2022

Serikali imetenga kitita cha dola elfu 22,000 zaidi ya Sh 50 Milioni kwa wanamichezo watakaotwaa medali ya fedha, dhahabu, na shaba kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kuanza tarehe 28 Julai hadi 08 Agosti, 2022 nchini Uingereza.

Msafara wa Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola umeagwa,

Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mohammed Mchengerwa amesema wametenga bonusi kwa washindi ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.

"Kila atakayeleta medali ya dhahabu atapewa bonasi ya dola 10,000, medali ya fedha dola 7000 na medali ya shaba dola 5000," amesema

Waziri Mchengerwa amesema leo Julai 20, 2022 wakati wa kuziaga na kuzikabidhi bendera timu ya Tanzania zinazokwenda kwenye michezo hiyo na ili ya mchezo wa kabaddi inayoshiriki michezo ya Afrika nchini.

"Tanzania tunaweza, inawezekana,"alisisitiza Waziri Mchengerwa.

Amesema Serikali imetimiza wajibu wao na TOC pia imetimiza wajibu wao katika maandalizi wa timu hizo.

"Nendeni mkaliheshimishe taifa," amesema waziri Mchengerwa.