Jumatano , 23rd Aug , 2017

Mtanange wa Simba na Yanga umekwisha huku Simba SC ikiibuka na ushindi wa Ngao ya Jamii kwa mwaka 2017 huku ikiwalaza watani zao kwa penati 5-4 huku wakiwa wamesawazisha historia ya kila mmoja kuchukua ushindi huo mara 2.

Katika mchezo huo uliobeba hisia za wapenda soka wengi dakika 45 za mwanzo zilimalizika huku timu zote zikiwa hazijaambulia chochote ambapo timu ya Simba SC ikionekana kumiliki mpira kwa asilia 58 huku Yanga wakitawala kwa asilimia 42.

Hata hivyo mpaka inafika dakika ya 90  timu zote mbili yaani siyo Simba wala Yanga aliyeweza kuona lango la mwenzake huku kumbukumbu za mwaka 2010 zikiwa zimejirudia kwenye historia kwa kumaliza dakika zote tisini na kwenda kwenye hatua ya matuta.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Refa Heri Sasii umekuwa wa hisia sana, kikosi cha Yanga kikiwa kwenye mfumo wa 1-4-3-3 huku Simba wakikimbiza kwa mfumo wa 4-4-2

Akizungumza baada ya mchezo huo Nahodha wa Yanga SC Haroub Cannavaro amewapongeza vijana wake baada ya mchezo huo na kusema kwamba "Vijana wangu wamejitahidi sana japokuwa bahati haikuwa ya kwetu. Nawapongeza kwa kazi kubwa waliyofanya lakini matuta ni mchezo wa kubahatisha na bahati wamepata Simba na ninawapongeza. Tunachotazama sasa mbele ni ligi kuu.

Kwa upande wa penati za Simba zilipigwa na Method Mwanjali, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Mohamed Hussein huku Penati ya ya nyongeza iliyopigwa na  Mohamed Ibrahim ikiwapa Simba ushindi.

Hata hivyo penati za Yanga zilipigwa na Kelvin Yondani, Tshishimbi, Kamusoko, Ibrahim Ajib, Donald Ngoma,Ngoma pamoja na Husen Tshabalala