Jumatatu , 13th Nov , 2017

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu ya Yanga, imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi mwakani.

Yanga kupitia taarifa yake imesema imepokea barua ya mwaliko kutoka chama cha soka visiwani Zanzibar ZDFA kupitia kwa shirikisho la soka nchini TFF, na wameupokea mwaliko huo hivyo watashiriki kwenye michuano hiyo.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwakani kuanzia Januari 2 na kufikia kilele Januari 13 ambapo jumla ya timu 10 zitachuana kumsaka bingwa.

Timu hizo ni pamoja na Mbaingwa watetzi Azam FC, Yanga SC NA Simba SC. Timu kutoka Zanzibar ni JKU, Zimamoto, Taifa Jang’ombe, Mlandege, Shaba SC na Jamhuri. Hata hivyo ZDFA bado haijaitaja timu moja kutoka nchi za Uganda au Kenya mabyo itashiriki michuano hiyo.

Michuano ya mwaka huu Yanga iliondolewa na mahasimu wao Simba katika hatua ya nusu fainali, kabla ya Simba kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC ambao waliibuka mabingwa.