Yanga kutua Ruvuma Alhamisi

Wednesday , 13th Sep , 2017

Mabingwa wa soka nchini timu ya Yanga imeendelea na mazoezi ya kujiwinda na mchezo wake wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Majimaji ya Songea.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema timu hiyo imeendelea na mazoezi leo mjini Njombe. Kambi hiyo ya Njombe itafikia tamati alhamisi Sep 14, ambapo timu itasafiri kuelekea Ruvuma tayari kwa mchezo wake wa mzunguko wa tatu katika ligi kuu ya soka Tanzania bara VPL.

"Kwasasa timu ipo mjini Njombe inaendelea na kambi hadi siku ya alhamisi itakaposafiri kuelekea Ruvuma kwaajili ya mchezo wetu na Majimaji." amesema Dismas Ten.

Yanga inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 4 baada ya kutoa sare dhidi ya Lipuli FC na kisha kushinda dhidi ya Njombe Mji.