Jumapili , 22nd Oct , 2017

Klabu ya soka ya Wydad Casablanca imetinga hatua ya fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuitupa nje USM Alger kwenye nusu fainali.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Wydad Casablanca kucheza fainali hiyo tangu mwaka 2011. Mshambuliaji Achraf Bencharki alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-1 jana usiku huku bao la tatu likifungwa na Walid El Karti.

Mchezo wa jana kati ya Wydad Casablanca na USM Alger ulikuwa ni wa marejeano baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa huko Algeria wiki mbili zilizopita.

Wydad Casablanca itasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia na Ah Ahly ya Misri ili kujua itacheza na nani kwenye fainali. Katika nusu fainali ya kwanza Etoile du Sahel ikiwa nyumbani iliibuka na suhindi wa mabao 2-1 na leo itakuwa nchini Misri kusaka nafasi ya fainai mbele ya Ah Ahly.