Jumanne , 26th Sep , 2017

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameilalamikia ratiba ya ligi kuu ya England kuwa haimtendei haki wakati huu ambapo timu ina mechi za michuano ya Europa League.

Wenger amesema ratiba hairuhusu wachezaji kupumzika hali ambayo inaweza kusababisha timu yake kufanya vibaya. “Kucheza EPL Jumatatu kisha ukacheza Europa Alhamisi na EPL tena Jumapili haiwezi kuwa ratiba inayozingatia usawa”, amesema Wenger.

Usiku wa jana Arsenal imecheza mchezo wa ligi kuu ya EPL dhidi ya West Bromwich Albion na kushinda mabao 2-0 yakifungwa na Alexandre Lacazette.

Baada ya mchezo huo Arsenal itasafiri leo kuelekea Belarus kwaajili ya kuivaa FC BATE Borisov kwenye mchezo wa Europa League siku ya Alhamisi. Baada ya hapo Arsenal itarejea nyumbani na kuivaa Brighton and Hove Albion siku ya Alhamisi.