Jumanne , 23rd Mei , 2017

Golden State Warriors walijihakikishia kusonga mbele kuingia fainali ya NBA msimu huu baada ya kuwafunga San Antonio Spurs point 129-115 alfajiri ya kuamkia leo

Golden State Warriors Vs San Antonio Spurs

Warriors walitarajiwa kuwachapa  Spurs, hususani baada ya Kawhi Leonard wa San Antonio Spurs kupata jeraha lililomfanya ashindwe kuendelea na mchezo huo, na kutoa mwanya Warriors kuibuka machampioni wa ukanda wa Magharibi kwa ushindi wa mechi nne mfululizo (4-0).

Katika mchezo huo, nyota wa Warriors Stephen Curry amefanikiwa kufunga point 36 na kuifanya timu hiyo kuweka historia mpya katika ligi hiyo kwa kushinda michezo 12 mfululizo bila kupoteza

Baada ya ushindi huo, sasa Warriors wanawasubiri washindi wa ukanda wa Mashariki kwa ajili ya michezo ya fainali ya NBA ambako Cleveland Cavaliers wanaoongoza kwa ushindi wa mechi 2-1 dhidi ya Boston Celtics, na alfajiri ya kuamkia kesho watakuwa dimbani kwa ajili ya mchezo wa nne.