Ijumaa , 23rd Jun , 2017

Mchezaji wa Kimataifa wa kutoka Kenya anayechezea klabu ya Tottenham Hotspurs, ya ligi kuu ya soka nchini Englad, Victor Wanyama, leo anatarajiwa kuwa mgeni kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EA TV, kuanzia saa 3:00 usiku.

Victor Wanyama

Wanyama ambaye yupo nchini Tanzania kwa mapumziko, anatarajiwa kuja kuwafahamisha vijana hatua mbalimbali alizopitia hadi kufanikiwa kwenye maisha ya mpira wa miguu, mchezo amabao umekitajirisha vijana wengi duniani, hasa wanapopata nafasi za kucheza kwenye vilabu vya barani Ulaya.

Wanyama ukiwa ndiyo msimu wake wa kwanza kwenye klabu ya Tottenham, amekuwa mchezaji muhimu kwenye eneo la kiungo cha ukabaji, na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Chelsea kwenye ligi ya EPL, na hivyo kupata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya, msimu ujao.

Wanyama aliyezaliwa miaka 25iliyopita alisoma Kamukunji High School, shule ambayo ilikuwa na vipaji vya soka, na baadae alichezea vilabu vya ligi kuu ya soka nchini Kenya Nairobi City Strs na AFC Leopards.

Safari ya kucheza soka Barani Ulaya ilikuwa na changamoto nyingi sana, lakini ukifuatiliwa FNL leo usiku saa 3, utajua alipenyaje kufika huko.

Lakini kubwa zaidi Nahodha huyu wa timu ya Taifa ya Harambee Stars anakumbukwa kama ndiye Mkenya wa kwanza kufunga goli kwenye ligi ya mabingwa Barani Ulaya, wakati Celtic ya Scotaland ikiifunga Barcelona ya Hispania 2-1, Novemba 7 mwaka 2012.