Jumanne , 25th Jan , 2022

Timu ya wananchi na vinara wa Ligi kuu Tanzania bara Yanga SC imewapa mapumziko ya siku 1 wachezaji wake baada ya kikosi hicho kurejea kutoka jijini Arusha jana na wanatarajiwa kurejea tena kambini kesho Jumatano mchana tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbao FC.

wachezaji wa Yanga Saido Ntibanzokiza kushoto akiwa na Yennick Bangala kulia

Kikosi cha Yanga kilirejea Dar es salaam jana kikitoa Arusha ambako kilicheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na Dikson Ambundo. Na wanarejea Dar es salaam baada ya kucheza michezo miwili ugenini.

Kabla ya mchezo wa Polisi Tanzania walioucheza Januari 23, Januari 16 walicheza na Costal Union mjini Tanga na walishinda 2-0. Baada ya ushindi huo wa michezo miwili ugenini mfululizo kikosi cha timu ya wananchi kinaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 10 kikiwa na alama 35 wakifuatiwa na Simba wenye alama 25 wakiwa nafasi ya pili.

Wachezaji wa Yanga watarejea kambini kesho baada ya siku ya leo kupumzika na watakaporejea itakwa ni maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC mchezo utakao chezwa Januari 29 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.