Jumatatu , 28th Sep , 2020

Raundi ya nne ya Ligi kuu Tanzania bara kukamilika leo kwa mchezo mmoja utakao chezwaJijini Tanga katika dimba la Mkwakwani.

Coastal Union haijashinda mchezo hata mmoja na haijafunga goli katika michezo mitatu ya Ligi kuu iliyocheza mpaka sasa

Coastal Union ya Tanga wanawaarika JKT Tanzania ya Dodoma katika mchezo utakao chezwa majaira ya saa 10 jioni.

Coastal chini ya kocha Juma Mgunda haijashinda mchezo hata mmoja katika michezo mitatu iliyocheza mpaka sasa wamefungwa michezo miwili na wamesare mchezo mmoja na kikosi hicho hakijafunga bao hata moja huku wakiwa wameruhusu mabao matatu.

Mchezo wa jioni ya leo ni wa pili wanacheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani, mchezo uliopita katika Dimba hilo walitoka sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC, Coastal wapo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama moja.

JKT Tanzania wanacheza mchezo wa tatu ugenini msimu huu tukiwa katika michezo ya raundi ya nne, kwenye michezo miwili iliyopita wakiwa ugenini wamefanikiwa kuondoka na jumla ya alama 4, wakiwa ugenini waliifunga Kagera Sugar bao bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, na waliodoka na alama moja kwenye mchezo ulipipita dhidi ya Polisi Tanzania baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kikosi JKT chini ya kocha Abdallah Mohamed “Bares” kimeshinda mchezo mmoja wamesare mchezo mmoja na wamepoteza mchezo mmoja wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama zao 4.

Msimu uliopita JKT Tanzania walifanikiwa kuondoka na alama 4 mbele ya Coastal Union kwa kuifunga mchezo mmoja na mchezo mmoja walitoka sare, na ushindi huo JKT waliupata katika Dimba la Mkwakwani ambako mchezo wa jioni ya leo utachezwa.