Jumatatu , 20th Mar , 2017

Shirikisho la Soka nchini TFF limesema, wadau husika wa deni wanaodaiwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA ambao ni pamoja na serikali pamoja na klabu yaYanga, wanaendelea na mazungumzo ili kuweza kuafikiana juu ya deni hilo.

Ofisi za TFF bado zimeendelea kushikiliwa na TRA

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema deni hilo linawahusu pia wadau hao (Yanga na serikali) na kwamba TRA haikuweza kuwadai Yanga moja kwa moja kutokana na mdau mkubwa ambaye ni TFF kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia suala hilo.

"Deni hili linatokana na Yanga katika mchezo wa msimu uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ambapo mashabiki waliingia bure na serikali iliangalia watu sasa katika kupiga hesabu ya watu walioingia Uwanjani Serikali haikuweza kuwasiliana na Yanga moja kwa moja kwa ajili ya fedha zinazotakiwa, hivyo ikaangalia chombo chenye muunganiko na Yanga ambao ni sisi TFF" Amesema.

Alfred Lucas

Kuhusu serikali, Lucas amesema "Suala lingine ni la Timu ya Taifa ya Brazili mbayo ilikuja nchini mwaka 2010 na kabla ya hapo kuna suala pia la aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Marcio Maximo,"