Jumatano , 16th Aug , 2017

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea malalamiko kutoka Kagera Sugar dhidi ya Azam FC, kuhusu mchezaji Mbaraka Yussuf aliyesajiliwa na Azam Fc.

Mchezaji Mbaraka Yusuph

Kagera Sugar imeilalamikia Azam FC kwa kitendo cha kumsajili mchezaji wao Mbaraka Yussuf, ambaye bado hajamaliza mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Timu ya Azam kwa upande wao wamesema walimsajili mchezaji huyo kwa kuwa mkataba wake ulionyesha ulikuwa wa mwaka mmoja na tayari ulikuwa umeisha, wakati Kagera wamesema walikuwa na mkataba wa miaka mitatu na mchezaji huyo, hivyo ulikuwa ndani ya muda.

Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kinatarajiwa kuketi Jumapili kupitisha usajili, lakini kabla kitapitia malalamiko hayo na kuchukua uamuzi.

Jana Agosti 14, 2017 ilikuwa siku ya mwisho kwa timu na vituo vya kuibua na kukuza vipaji kuwasilisha malalamiko yao TFF kuhusu fidia za mafunzo, ada ya usajili, ada za maendeleo na kuvunjwa kwa mikataba kutoka katika timu walizochezea hadi msimu uliopita.