Jumanne , 12th Sep , 2017

Shirikisho la soka nchini TFF, limetangaza neema kwa makocha ikiwa ni sehemu ya kuboresha kiwango cha soka nchini kwa kupatikana kwa wataalam wengi wa ufundi.

Kupitia kwa msemaji wa shirikisho hilo Alfred Lucas, TFF imethibitisha kuwa inaendesha kozi ya ukocha katika ngazi ya awali (Preliminary) pamoja na ngazi ya kati (Intermidiate).

Kozi hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano na mikoa ya Songwe, Lindi na Kigoma. Katika wilaya ya Songwe kozi ya awali inaongozwa na Mkufunzi John Simkoko wakati wilayani Tunduma kozi hiyo inaendeshwa na mkufunzi George Mkisi.

Mkoani Kigoma kozi mbili zinaendeshwa ambapo kozi ngazi ya awali inaendeshwa na mkufunzi George Komba wakati Rogasian Kaijage anaendesha kozi ngazi ya kati.

Mkoani Lindi kozi ngazi ya awali imeanza jana Sep 11, 2017 wilayani Lindi chini ya mkufunzi Michael Bundala.