Jumatatu , 28th Sep , 2020

Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea kurindima katika raundi yake ya nne ambayo itakamilishwa kwa mchezo mmoja utakaopigwa leo huko CCM Mkwakwani Mkoani Tanga ambapo Coastal Union itakua mwenyeji wa maafande wa JKT Tanzania,lakini tumekuandalia takwimu muhimu tangu kuanza kwa msimu huu.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone (Pichani) akijiandaa kupiga mpira wa kona, ni mmoja ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao( 4) hadi sasa.

-Azam ndiyo Timu pekee iliyokusanya alama zote katika mechi nne za VPL 12, imeshinda mechi 4, imefunga mabao 5 na ndiyo Timu pekee ambayo haijaruhusu bao katika ligi kuu.

-David Kisu ndiye mlinda mlango ambaye hajaruhusu bao katika VPL katika mechi 4, na kuisaidia Azam kushinda bila wavu wake kutikisikika, akifuatiwa na Metacha Mnata wa Yanga ambaye hajaruhusu bao katika mechi tatu alizoanza.

-Simba ndiyo Timu pekee iliyofunga mabao mengi zaidi katika ligi kuu (10), imeruhusu mabao (2) , ikifuatiwa na KMC iliyofunga mabao (8) .

-Timu za Gwambina, Mbeya City na Coastal Union ndio Timu pekee ambazo hadi sasa hazijafunga goli hata moja katika ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.

-Mbeya City ndio Timu pekee iliyofungwa mechi zote 4 za VPL na imeruhusu mabao mengi zaidi katika ligi kuu (7).

-Ni Timu nne kati ya 18 ambazo hazijapata ushindi katika ligi kuu ambazo ni Coastal Union (Tanga ,Gwambina (Mwanza, Mwadui(Shinyanga na Mbeya City (Mbeya).

-Hadi sasa ni Timu Tatu pekee ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja katika VPL,Azam imeshinda 4,Simba imeshinda 3,sare 1,Yanga imeshinda 3 sare 1.

-Prince Dube wa Azam ndiye kinara wa kupachika mabao katika ligi kuu, amefunga mabao matatu huku akitoa assissts 1.

-Chriss Mugalu wa Simba amefunga bao 2 katika mechi 2 alizoicheza katika VPL,pia kafunga bao 4 katika michezo yote minne aliyopewa nafasi.