Jumatano , 28th Jun , 2017

Mamlaka ya kuzuia na kuapambana na Rushwa nchini Takukuru imethibitisha kwamba inafanya uchunguzi wa madai ya rushwa kunako shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Rais wa TFF Jamali Malinzi Kushoto na kupande wa kulia ni Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa

Afisa uhusiano wa TAKUKURU Mussa msalaba ameiambia East Africa Radio kwamba wanafanya kazi hiyo kwa kufuata utaratibu na kanuni zilizopo hivyo watatoa taarifa rasmi mara baada ya kukamilisha kazi yao

Ufafanuzi huo wa TAKUKURU unafuatia uwepo wa taarifa za kushikiliwa kwa raisi wa TFF Jamali Malinzi sambamba na katibu mkuu wa shirikisho hilo Mwesigwa Celestine kwa mahojiano ambayo hayajulikana yanahusiana na nini.

Katika hatua nyingine, msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara (aliyefungiwa) ametuma salamu za pole kufuatia sakata hilo kwa Shirikisho hilo kwa kusema hizo ni changamoto tu katika maisha.

"Poleni viongozi wangu wa TFF, 'no matter what' ni challenges' tu katika 'life', binadaamu hatufai kuombeana mabaya,hata kama huwakukutendea haki, Mungu awasimamie kutendewa haki" aliandika Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram