Alhamisi , 9th Nov , 2017

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeondoka nchini leo Alhamisi Novemba 9 kwenda nchini Benin kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Fifa.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amewaambia waandishi wa habari kuwa kuwa wachezaji wote wameshaingia kambini kasoro Nahodha, Mbwana Samatta ambaye ni majeruhi pamoja na Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.

“Kikosi cha timu yetu ya taifa kimeondoka kwenda Benin kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki na kitakapofika rasmi kesho itaendelea na programu yake mazoezi huko Benin,” alisema Lucas.
 

Taifa Stars inakwenda Benin bila ya Nahodha wake, Mbwana Ally Samatta ambaye ameumia goti na atatakiwa kukaa nje kwa wiki sita akipata matibabu.