Ijumaa , 30th Oct , 2020

Klabu ya Liverpool imethibitisha kwamba zoezi la upasuaji wa goti la mlinzi wake Virgil van Dijk limefanyika kwa mafanikio.

Mlinzi wa Liverpool, Virgil van Dijk alipoumia katika mchezo dhidi ya Leicester City.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hajacheza tangu apate jeraha la mishipa ya mbele ya goti lake baada ya kugongana na kipa wa Everton Jordan Pickford kwenye sare ya 2-2 ya Ligi Kuu mnamo 17 Oktoba.

Liverpool ilisema hakuna muda uliowekwa juu ya kurudi kwa uwanjani kwa raia huyo wa Uholanzi ingawa ilikadiriwa kuwa huenda akakaa nje kwa zaidi ya miezi nane.

Kikosi cha Jurgen Klopp pia kilimpoteza Fabinho, ambaye anatajwa atakaa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Fc Midtyland katikati mwa juma.