Ijumaa , 30th Oct , 2020

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amehoji ni kwanini vilabu vya Ligi Kuu England vilipiga kura ya kupinga kufanya mabadiliko ya wachezaji wa 5 kwenye michezo ya EPL msimu huu.

Mchezo dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili utakuwa wa 100 kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer akiisimamia Man United kama kocha mkuu

Kura ya vilabu kupinga kanuni ya kufanya mabadiliko ya wachezaji wa 5 kwa mchezo mmoja ilipigwa mwezi Agosti na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu England EPL na kutumia kanuni ya zamani ya kufanya mabadiliko ya wachezaji wa 3.

Lakini kanuni hiyo bado inatumika kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya na ile ya Europa league.

“Sielewi na siamini kwanini ilipigwa kura ya kupinga, tunapaswa kuwalinda na kuwafikiria wachezaji ” alisema Solskjaer alipokuwa akiongeza na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Arsenal.

Kutokana na mlipuko wa Covid-19 ambao ulisababisha ligi mbali mbali kusimama Duniani kote na wachezaji kushinda kufanya mazoezi, ili kulinda afya za wachezaji kuwaepusha na majeruhi, vilabu vilipewa nafasi ya kufanya mabadiliko ya wachezaji wa 5 kwa mchezo kutoka wa 3.

Shirikisho la soka Dunia FIFA lilitoa ruhusa kwa ligi mbali mbali kendelea kutumia kunani hiyo kwa muda mpaka mwishoni mwa msimu huu wa 2020-21, lakini vilabu vya England vilipiga kura ya kupinga kununi hiyo na kutumia kanuni ya zamani ya mabadiliko ya wachezaji wa 3.

Ole Gunnar sio kocha wa kwanza kuhoji juu ya umuhimu wa mabadiliko ya wachezaji wa 5 kwani hata Kocha wa Manchester City Pep Guardila anaamini afya za wachezaji zinapaswa kulindwa huku Kocha wa Chelsea, Frank Lampard akisisitiza makosa yalifanyika kupinga kanuni ya mabadiliko .