Jumapili , 23rd Apr , 2017

Tegemeo la watanzania Alphonce Felix Simbu ameshika nafasi ya tano kwenye mbio za London Marathon zilizofanyika leo jijini London.

Daniel Wanjiru kutoka Kenya aliibuka kinara wa mbio hizo akitumia muda wa saa 02:05:48, nafasi ya pili ikichukuliwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia aliyetumia muda wa saa 02:05:57.

Nafasi ya tatu ya mbio hizo imeenda kwa mkenya mwingine Bedan Karoki aliyetumia muda wa saa 02:07:41, nafasi ya nne ikaenda kwa mkenya Abel Kirui akitumia muda wa saa 02:07:45, na namba tano ikienda kwa mtanzania Alphonce Simbu aliyetumia muda wa saa 02:09:10.

Timu ya East Africa TV & Radio inapenda kutoa pongezi kwa Alphonce Simbu kwa hatua aliyofikia.