Alhamisi , 16th Sep , 2021

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na wadhamini wao wametambulisha Mascot rasmi wa klabu hiyo watakaojulikana kama Mo rafiki kwa lengo la kuongeza hamasa pindi timu iwapo uwanjani kwenye mechi mbalimbali kuanzia msimu 2021/22.

Picha ya Mascot wa klabu ya Simba

Akieleza leo mbele ya waandishi wa Habari, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzales amesema, Mascot hao watakuwa wakihudhuria mechi za Simba popote nchini kuanzia kwenye tamasha la Simba Day mwaka huu lakini pia watatumika kujenga ukaribu na kuwahamasisha watoto kupenda mchezo wa mpira.


Simba itacheza mchezo wa kirafiki na klabu ya TP Mazembe kutoka jiji la Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwenye  kilele cha maadhimisho ya Simba Day Septemba 19 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa