Simba Yanga shughuli pevu nusu fainali Mapinduzi

Jumatatu , 11th Jan , 2021

Nusu fainali mbili za Kombe la Mapinduzi, zinachezwa leo Jumatatu Januari 11, 2021, katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, ambapo michezo yote miwili ya hatua hii itapigwa.

Wachezaji wa Simba SC na Namungo FC

Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Yanga dhidi ya Azam majira ya saa 10:00 jioni na usiku majira ya saa 8:15 kutakuwa na nusu fainal ya pili inayohusu Simba dhidi ya Namungo. Washindi watakutana katika fainali Jumatano tarehe 13/1/2021.

Michuano hii iliyoanza  5/1/2021 ilishirikisha  timu 9,  tano kutoka  bara  ambazo ni Simba, Yanga, Namungo, Mtibwa na Azam, huku visiwani wakiwa na timu nne  Jamuhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi, lakini katika hatua ya nusu fainali hizi, zimehusisha timu zote kutoka Tanzania Bara.

Kikosi cha Yanga SC na wachezaji baadhi wa Azam FC 

Aliyekuwa bingwa mtetezi Mtibwa Sugar, ametolewa rasmi katika mashindano haya, baada ya kuruhusu  kupoteza mchezo mmoja na kushinda moja hivyo kukosa tiketi ya 'mshindwa bora'.

Mashindano haya yaliyoanza mwaka  2007 yameshuhudia timu za  Tanzania bara zikifanya vyema zaidi kwa kutwaa ubingwa mara 10 katika misimu 13 ya mashindanano, Azam mara 5 Simba 3 Yanga 1 na Mtibwa mara 1.