Simba waomba kuandamana Jumanne

Friday , 21st Apr , 2017

Klabu ya Simba leo imeandika barua kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuomba kufanya maandamano ya amani siku ya Jumanne ya tarehe 25 mwezi huu

Rais wa Simba, Evans Aveva

Imesema lengo ya maandamano hayo ni ili kupeleka ujumbe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kuwa klabu hiyo imekuwa ikionewa na kutotendewa haki na shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa Simba Evans Aveva ambayo imekwenda kwa jeshi la polisi wameomba kufanya maandamano hayo ya amani ambayo yatakwenda mpaka kwa Waziri na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Katika taarifa hiyo, Simba inaendelea kusisitiza kuwa klabu hiyo imeendelea kuonewa huku malalamiko yake mengi yamekuwa hayafanyiwi kazi kwa haraka.

Hii ndiyo barua yao.......

 

Recent Posts

Rais Magufuli akipokea Taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.

Current Affairs
Jinsi Tanzania inavyoibiwa madini

Mohamed Mchengerwa - Mbunge wa Rufiji

Current Affairs
Wananchi wamekondeana - Mchengerwa

Wawakilishi wa timu shiriki wakishuhudia droo pamoja na kupata semina maalum kuelekea michuano hiyo

Sport
Ratiba Sprite Bball Kings yawekwa hadharani

Simba na Yanga walipokutana msimu huu

Sport
Audio: Simba na Yanga kuwania milion 60