Jumatatu , 14th Aug , 2017

Mwenyekiti wa baraza la Wadhamini Simba 'Mzee Kilomoni' amesimamishwa uanachama na Klabu hiyo ikiwa ni baada ya kudaiwa kuvunja katiba ya Simba  kwa kupeleka mambo ya soka Mahakamani ilhali kuna chombo maalum cha kusuluhisha matatizo klabuni hapo.

Mchezaji Emmanuel Okwi

Katika mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo ilimsimamisha uanachama Mzee Kilomoni huku hukumu ikiwa imependekezwa na Kaimu Rais Simba, Salim Abdallah 'Try Again' katika mkutano huo mbele ya waachama 927 waliyohudhuria, kuwa Kilomoni aondolewe katika Baraza la Wadhamini la Simba kwa kitendo cha kufungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita.

Hata hivyo baada ya Klabu hiyo kumaliza tukio hilo ilielekea uwanjani ambapo timu ya Simba iliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliyopigwa siku ya Jumapili (Jana) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Balo la Simba lilifungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza ikiwa ni masaa machache tangu klabu hiyo itoke kwenye mkutano mkuu.

Matokeo hayo ni mwendelezo wa matokeo mazuri iliyopata klabu hiyo ikiwa siku chache tangu ilipoifunga Rayon ya Rwanda bao 1-0 katika mchezo wa Simba Day.