Jumanne , 25th Jan , 2022

Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Simba SC kimeondoka Jijini Dar es salaam leo asubuhi kuelekea mkoani Kagera ambako kitacheza mchezo wa Ligi Kuu kesho Januari 26, 2020 dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wa Simba SC wakipanda ndege tayari kwa safari ya kuelekea Kagera

Kwa mujibu wa taarifa kikosi cha Simba kimeondoka na kikosi kamili kuelekea kwemnye mchezo huo wa Ligi ambao ni wa kiporo wa raundi ya 9. Kikosi hicho cha wekendu wa msimbazi kilifanya mazoezi ya mwisho jana Dar es salaam na inategemewa leo baada ya kufika Bukoba leo kitafanya tena mazoezi kwenye uwanja wa Kaitaba.

 

Wachezaji wa Simba Meddie Kagere Kulia akiwa na Sadio Kanoute kushoto wakiwa uwanja wa ndege wa Mawalimu Nyerere Dar es salaam

Kwenye michezo 2 ya mwisho Simba waliocheza kwenye uwanja wa Kaitaba imeshinda michezo yote ikiwemo ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa msimu uliopita mabao ambayo yalifungwa na Chris Mugalu na Luiz Jose Miqueson.

Simba wanaelekea kwenye mchezo huu wakiwa wameshinda michezo 2 tu kwenye michezo 5 ya mwisho na michezo miwili ya mwisho wamefungwa 1 na sare 1 wakati Kagera wameshinda mchezo 1 kwenye michezo 5 ya mwisho.