Jumapili , 23rd Apr , 2017

Siku moja baada ya kutangaza maandamano ya amani ambayo yangefanyika siku ya Jummane tarehe 25 mwezi huu. Klabu ya Simba imeamua kusitisha maandamano hayo baada ya kuona nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia sintofahamu inayoendelea b

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara

Siku moja baada ya kutangaza maandamano ya amani ambayo yangefanyika siku ya Jummane tarehe 25 mwezi huu. Klabu ya Simba imeamua kusitisha maandamano hayo baada ya kuona nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia sintofahamu inayoendelea baina yao na Shirikisho la Soka nchi (TFF). 

Ikumbukwe juzi Simba iliandika kwa Jeshi la Polisi ikiomba kibali cha maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa na viongozi,wanachama na washabiki wa klabu, kwenda Wizara inayosimamia Michezo  ili kupeleleka kilio chao juu ya TFF, kwa namna inavyoshughulikia malalamiko ya klabu hiyo.