Jumapili , 24th Sep , 2017

Gavana wa zamani wa jimbo la California nchini Marekani Arnold Schwarzenegger jana ametembelea klabu ya Barcelona na kujionea mambo mbalimbali ndani ya Camp Nou.

Mwigizaji huyo wa Hollywood alikuwa mgeni maalum ndani ya uwanja wa Barcelona kabla ya mchezo wa ligi jana usiku ambapo Barcelona ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Girona.

Anord alitembelea maeneo mbalimbali ndani ya Camp Nou akijionea miundombinu na kumbukumbu za wachezaji waliowahi kuchezea klabu hiyo.

“Ni furaha kubwa kuwa hapa, ni klabu yenye historia kubwa na wachezaji wenye vipaji vikubwa, nimefurahi kuona makombe na video za zamani hakika imekuwa siku nzuri na ya kihistoria kwenye maisha yangu. Nitarejea tena”, alisema Anord.

Hii ni mara ya pili ndani ya miaka miwili kwa mkali huyo wa Terminator, Commando na Predator kutembelea jiji la Barcelona ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mradi wake wa Anord Classic Europe.