Jumapili , 23rd Jul , 2017

Nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta imeendelea kung’aa baada ya jana kuifungia timu yake ya Genk bao moja kwenye sare ya 1-1 waliyotoka na klabu ya Everton ya nchini Uingereza katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Ubelgiji

Mbwana Samatta

Wakiwa nyuma kwa bao moja lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, Samatta aliifungia Genk bao la kusawazisha dakika ya 55.
Huo unakuwa mchezo wa 63 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk  kutoka TP Mazembe ya DRC.