Jumatano , 20th Oct , 2021

Mshambuliaji hatai wa Liverpool, Mohammed Salah ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi kwenye historia ya klabu hiyo kwa kufikisha mabao 31 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pekee usiku wa jana.

(MO Salah akifunga kwa mkwaju wa Penalti (kwenye ociha kubwa) na Sebastien Haller (picha ndogo) akisheherekea baada ya kufunga bao)

Salah amefikia rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa  Liverpool wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa michuano hiyo.

Mbali na rekodi hiyo, Salah pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Liverpool kufunga magoli 11 katika michezo tisa mfululizo kwenye michuano yote ambayo Liverrpool imeshiriki akiwa amekosa mchezo mmoja tu.

Salah amevifunga vilabu vya Chelsea, Leeds, Milan, Crystal Palace, Brentford na FC Porto. Salah amekosekana kwenye mchezo  mmoja  tu msimu huu  dhidi ya Norwich  kwenye michuano ya Carabao ambao yeye hakujumuishwa kikosini.

Kwa upande mwingine,

Nyota wa Ajax, Sebastien Haller amezidi kuweka rekodi sawa na Erling Halaand kwa kufunga magoli sita kwenye michezo yake mitatu ya mwanzo akiwa na timu yake mpya kwenye msimu wa kwanza wa michuano hiyo mikubwa Duniani.

Haller aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao moja kwa ushindi wa Ajax wa mabao 4-0 dhidi ya Dortmund usiku wa jana na kuondoka kifua mbele kwenye usiku wa mabingwa wa ulaya.

Ikumbukwe kuwa Haller aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kwenye historia ya UCL kufunga mabao 4 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sporting CP na kuifikia rekodi ya Marco Van Basten wa AC Milan mwaka 1992