Jumamosi , 23rd Sep , 2017

Ligi ya Mabingwa Barani Afrika inatarajwa kuendelea hii leo kwa jumla ya michezo 3 kupigwa katika hatua ya robo fainali.

Mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wamesafiri hadi nchini Morocco kuvaana na Wydad Casablanca wakiwa na akiba ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo mwingine Esparance wapo nyumbani kwao jijini Tunis, Tunisia kuikaribisha Al Ahly ya Misiri wakiwa na jeuri ya sare ya mabao 2-2 waliyoipata ugenini nchini Misri na leo watakuwa wanaisaka nusu fainali kwa sare isiyozidi mabao 2 au ushindi wowote.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya USM Alger dhidi ya Ferroviario Beira ambapo katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1. Kesho kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Etoile du Sahel dhidi ya Ali Ahli Tripoli ya Libya.