Ratiba Kombe la Shirikisho yapanguliwa

Tuesday , 14th Feb , 2017

Raundi ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la TFF itaanza Februari 16, 2017 badala ya Februari 24, mwaka huu huku mechi kati ya Simba na African Lyon ikibadilishwa tarehe.

Siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Simba na African Lyon mchezo ambao awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017.

Raundi hiyo itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja ambao utakaopigwa saa 1.00 jioni.

Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Recent Posts

Rais Magufuli alipotembelea bandarini na kukutana na mchanga wa dhahabu uliokuwa tayari kusafirishwa nje ya nchi

Current Affairs
Rais Magufuli aunda kamati kuchunguza mchanga